

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Tunatoa pole kwa Menejimenti ya Wizara ya Uchukuzi, Familia, Na wote wanaoguswa na msiba wa Bw. Leonard Mutegeki Lwiza aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Uchukuzi.

Bodi ya Wakurugenzi na Menejiment ya Shirika la Reli kutoka nchini Uganda wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ndg. Al -Hajji Abdallatiff D. Wangubo, leo tarehe 27 Mei, 2025 wametembelea bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala ya muunganisho wa njia mbalimbali za usafirishaji pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda
Bodi hiyo imepokelewa na Mkurugenzi Wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.

Kikosi cha Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vikosi vya uokozi vya kiserikali na binafsi leo tarehe 22 Mei , 2025 limefanya zoezi la utayari wa kukabiliana na majanga ya moto lililofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam.
Meneja zimamoto na Usalama Bw. Mussa Biboze akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa wameweza kuudhibiti moto huo kwa muda mfupi zaidi wa dakika 15 tu.
Aidha amesema kuwa zoezi hilo lililenga kupima utayari katika mashirikiano ya vikosi vya uokozi iwapo itatokea majanga ya moto
Zoezi hilo limehusisha vikosi vya uokozi ambavyo viko chini ya TPA , vikosi mbalimbali vya usalama kama jeshi la zimamoto, Wanachi, Polisi pamoja na makampuni binafsi yanayojishughulisha na kuzima moto, huduma za dharula za uokozi na hospitali ya Taifa Muhimbili .