Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) tunaungana na Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kuadhimisha kumbukizi ya Siku ya Nyerere.
Tunaendelea kuuenzi daima mchango wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika maendeleo ya Taifa letu, kwa kuendelea kuboresha zaidi huduma za Kibandari ili kuongeza mchango wa Taasisi hii katika maendeleo ya Taifa na Nchi zinazohudumiwa na Bandari zetu.
#tpa#sikuyanyerere#nyerereday#kumbukiziyamiaka26
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania IGP Mstaafu Mhe. Balozi Ernest J. Mangu ameongoza wajumbe wa Bodi hiyo katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa, tarehe 10 Oktoba 2025.
Ziara hiyo ilihusisha kutembelea miundombinu ya Bandari na kupata taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Bandari hiyo ya kisasa ambao unatekelezwa na Kampuni ya CHEC ya Nchini China ili kushuhudia hatua na hali halisi ya mradi huo ilivyo kwa sasa.
Mhe. Balozi Mangu alieleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa Bandari hiyo ambayo inatarajiwa kuchakata zaidi ya Tani 60,000 za shehena ya samaki kwa mwaka mara itakapokamilika na kuanza kazi.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Kampuni ya CHEC Bw. Douglas Semwenda ameeleza kuwa, mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 266 ulianza kutekelezwa mwezi Septemba, 2023 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Februari, 2026.


Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja “Customer Service Week” Bandari ya Tanga Kitengo cha Tehama kimeendelea kutoa huduma bora kwa wateja kupitia mifumo.
Akizungumza juu ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba, Afisa Mwandamizi Kitengo cha Tehama Bandari ya Tanga Bw. Johanes Rwezaula alisema kuwa katika kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wateja miundombinu ya mawasiliano katika bandari hiyo yameimarika.
“Miundombinu ya mawasiliano imeboreshwa na mifumo imeimarika hakuna tena changamoto za mara kwa mara za kukatika kwa mtandao jambo ambalo limesaidia kurahisisha utendaji kazi katika utoaji wa mizigo na upatikanaji wa taarifa” Aliongeza Rwezaula.
Aidha pia Rwezaula alisema kuwa mifumo inayotumika bandarini ya ITOS na POAS ambayo imeunganishwa na mifumo ya Taasisi zingine kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama TANCIS na Wizara ya Fedha GePG imesaidia utendaji kazi bandarini, hivyo aliwataka wateja waendelee kufurahia huduma zinazotolewa bandarini hapo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) IGP Mstaafu Mhe.Balozi Ernest J. Mangu, ameongoza wajumbe wa Bodi hiyo katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa Bandari ya Mtwara, tarehe 9 Oktoba 2025.
Ziara hiyo ilihusisha kutembelea Bandari hiyo na kupata taarifa za utendaji kazi wake, pamoja na kutembelea Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao ili kushuhudia maendeleo ya utekelezaji wake.
Mhe. Balozi Mangu alieleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi huo, ambao unatarajiwa kuhudumia tani milioni 2.5 za shehena kwa mwaka utakapokamilika.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Dkt. Baraka Mdima, ameeleza kuwa TPA itaendelea kuzisimamia na kuziendeleza Bandari zote nchini, ikiwemo Bandari ya Mtwara, ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya huduma za bandari na kuiwezesha sekta ya bandari kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Akieleza matarajio yaliyopo, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Ferdinand Nyathi, amesema kuwa mwelekeo na mtazamo wa kimasoko kwa sasa ni chanya, kwa kuwa Bandari imeanza kuhudumia shehena ya mafuta yanayosafirishwa kwenda nchi jirani za Zambia na Malawi, hatua ambayo inazidi kufungua milango ya Bandari kwa kuhudumia shehena zaidi katika nchi hizo.


Katika kuhakikisha Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2025 “Mission Possible” inatekelezwa kwa vitendo, Bandari ya Tanga imejipanga kuilinda mizigo ya wateja ili iweze kutoka bandarini ikiwa salama.
Uhakikisho huo umetolewa na Afisa Ulinzi Mwandamizi wa Bandari ya Tanga Bw. Rajani Fidu Hussein katika mwendelezo wa wiki ya Huduma kwa Wateja alipokuwa anawahudumia huduma maeneo katika yake ya kazi.
Bw. Fidu alisema kuwa Bandari ya Tanga ni salama ulinzi wa mizigo ni wa uhakika, hivyo nawashauri wateja waendelee kutumia Bandari ya Tanga ambayo iko tayari kutoa huduma na kutatua changamoto za wateja usiku na mchana.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"