

Maofisa wa kijeshi kutoka nchini Nigeria wakiongozwa na Air Vice Marshal Titus Z. Dauda wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza masuala ya kiuchumi, siasa na kiutamaduni pamoja na mchango wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA katika maendeleo ya Kiuchumi nchini Tanzania.
Pamoja na Mambo mengine ujumbe uhuo ulipata fursa ya kutembelea kujionea shughuli za bandari ikiwemo gati ya kuhudumia magari 'Roro Terminal " Pamoja na gati 1-7
Ujumbe huo ulipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TPA Bw. Plasduce M. Mbossa.

Katika Mitandao ya Kijamii na makundi sogozi, zinasambaa taarifa potofu kwa njia ya sauti kuhusu kuwepo kwa taarifa za uwepo wa Shehena ya Silaha zinazosafirishwa kwenda Kalemie nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Bandari ya Kigoma. Kufuatia taarifa hizo potofu, Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzaia (TPA) inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo

Tanga, Machi 1, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuongeza ufanisi katika sekta ya bandari, ambayo ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa wito huo leo alipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gati mbili mpya, unaolenga kuboresha uwezo wa bandari hiyo kushindana kimataifa.
“Bandari ni ushindani. Ni lazima mfanye kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa ili tuweze kuongeza ufanisi na kuvutia biashara zaidi,” alisema Mhe. Rais Dkt. Samia.
Ameeleza kuwa maboresho yanayoendelea katika bandari mbalimbali nchini yanahitaji watumishi wa TPA kuwa na ujuzi wa kisasa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia, hivyo amewahimiza kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza ufanisi na ushindani katika bandari.
Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia ameagiza Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TPA kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na haki, akisisitiza kuwa hatavumilia vitendo vyovyote vinavyoweza kuhujumu uchumi kupitia bandari.
“Nimeridhishwa na hatua kubwa ya maboresho yanayoendelea katika bandari zetu, ikiwemo Bandari ya Tanga. Lazima tuhakikishe uwekezaji huu unawanufaisha Watanzania kwa kupunguza gharama za biashara na kuongeza ufanisi wa huduma,” aliongeza.
Akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, alimpongeza kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya bandari, akieleza kuwa uwekezaji unaoendelea umekuwa na matokeo chanya kwa uchumi wa nchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa, alimweleza Mhe. Rais kuhusu hatua za utekelezaji wa mradi wa gati mbili mpya katika Bandari ya Tanga, akibainisha kuwa mradi huo utaongeza ufanisi wa upakuaji na upakiaji wa shehena.
Katika kutambua mchango wake wa kuimarisha sekta ya bandari, Bw. Mbossa alimkabidhi Mhe. Rais Tuzo ya Shukrani kwa uongozi wake thabiti na maelekezo yenye tija katika kuendeleza miundombinu ya bandari na kukuza uchumi wa Taifa.

Baraza la Majadiliano (JIC) la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Kituo cha Bandari ya Dar es Salaam limefanya kikao cha kawaida cha pili (2) kinachofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Kikao hiko cha siku (3) kimeanza tarehe 27 Februari 2025 ambapo kimelenga Kupitia na kuthibitisha kumbukumbu za kikao Na.1/2024/2025 cha Baraza la majadiliano ‘JIC’ kilichofanyika tarehe 16 mpaka 17/10/2024.
Kikao hiko kimeongozwa na Meneja Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mussa Biboze kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus.

Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Jumuiya ya Ulaya umekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kikao kilicholenga kuangalia namna bora ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na Bandari za Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya TPA Februari 25,2025 jijini Dar es Salaam,Kiongozi wa Ujumbe huo Mhe.Barry Andrews amesema Ujumbe huo unalengo la kuangalia ni njia zipi nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya zinaweza kutumia ili kuendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Bandari za Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce Mbossa ametumia fursa hiyo kuueleza Ujumbe huo mpango wa TPA wa miaka minne kuwa ni kuendelea kuimarisha miundombinu ya kufanyia kazi za kibandari na kuiunganisha Bandari na miundombinu ya reli na barabara ili kurahisisha usafirishaji wa shehena kutoka bandarini.
- MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DODOMA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)
- WAZIRI WA UCHUKUZI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MRADI MATENKI MAALUM YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA MAFUTA (OIL TERMINAL)
- SERIKALI YA UINGEREZA YAFURAHISHWA NA KUIPONGEZA SERIKALI KWA MABORESHO BANDARI YA DAR ES SALAAM
- TPA YAIBUKA MSHINDI KATIKA KUFUATA MIONGOZO NA KANUNI ZA e-GA