Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatekeleza jukumu la kusimamia na kutoa huduma za Bandari pamoja na kuhamasisha matumizi na kuendeleza miundombinu ya bandari.
Aidha katika kuhamasisha matumizi, uendelezaji na usimamizi wa bandari na maeneo yake ya ndani TPA huingia mikataba na taasisi nyingine kwa madhumuni ya kukasimu mamlaka ya utoaji wa huduma.
TPA ndio wanaoendesha mfumo wa Bandari zinazohudumia Tanzania Bara na nchi zisizo na Bandari za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda, Comoro na Zimbabwe.
Tovuti yetu ina taarifa, miongozo na taratibu za masuala yanayohusu Bandari na uendeshaji wake.