Cargo Service

Tuna zana, vifaa na mitambo ya kutosha kushughulikia shehena za aina mbalimbali. Timu zetu zenye wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali wanafanya kazi saa ishirini na nne kuhakikisha kuwa shehena zinazoingia na kutoka katika Bandari zetu ni salama wakati wote.

Aina za Mizigo Inayoshughulikiwa

01

Nafaka na Kichele

Hizi ni shehena kavu ambazo hazikujazwa kwenye magunia au vifungashio. Baadhi ya shehena hizi ni pamoja na aina mbalimbali za nafaka na malighafi. Nafaka hizo ni kama mchele, ngano,  mahindi, maharage. Malighafi ni bidhaa ambazo zina sifa mbili zinazofanana ambazo hazikujazwa kwenye magunia na zinaulinganifu, zenye kufanya shehena hiyo kuwa rahisi kushushwa au kumiminwa kwenye chombo cha usafirishaji. Bidhaa hizo ni kama makaa ya mawe,sukari, saruji, sodium nitrate, clinker, gypsum, shaba, makaa ya mawe, madini ya chuma na madini ya zinki.

02

Shehena Mchanganyiko

Hizi ni bidhaa zinazopakiwa moja moja, zikiwa ndani ya makasha. Shehena za aina hiyo zinazoshughulikiwa mara kwa mara na Mamlaka ya Usimamaizi wa Bandari Tanzania (TPA). Bidhaa hizo ni pamoja na chuma, chuma cha pua, makasha, metali, magari na sehemu za puli, trela, bidhaa za kilimo, mitambo, shaba, vichwa vya treni na sehemu ya vipuli, mabehewa, matrekta na sehemu ya vipuli.

03

Vimininika

Shehena ya vimiminika kama vile petrol, mafuta ya taa, dizeli, gesi, mafuta ya ndege na mafuta ya kula.