Bandari ya Mtwara na nyingine za Bahari ya kusini

Bandari ya Mtwara ni miongoni mwa Bandari kuu tatu zinazosimamiwa na mamlaka ya bandari Tanzania. Nyingine ni Dar es Salaam na Tanga. Bandari ya kina kirefu ya Mtwara ilijengwa kati ya mwaka 1948 na 1954. Uendelezaji wa bandari hiyo uliendana na ujenzi wa reli kuanzia Mtwara na Nachingwea. Kutokana na kufa kwa mradi wa kilimo cha Karanga, reli ilishindwa kutumika na hivyo imekufa na haifanyi kazi tena. Hata hivyo Bandari inaendelea kutumika lakini chini ya kiwango chake.

Sifa za Bandari

Gati la kina kirefu limesafishwa kufikia mita 9.5. hakuna masharti ya maji kupwa na maji kujaa kwa meli zinazoingia na kutoka bandarini. Lakini kuna masharti ya umbali wa mita 170 kutokana na umbo la mkondo hasa eneo la sehemu nyembanyemba ya ardhi iliyoingia baharini hasa MSEMO SPIT.

Eneo salama la kutia nanga lipo kwenye ghuba ya ndani lenye urefu wa mita 20. Hapa panaweza kutia nanga meli sita za urefu wa mita 175. Idadi ya meli inaweza kuongezeka iwapo mafungu mengi ya mchanga yataondolewa

Nyenzo za Bandari

Ukuta wa Gati

Bandari ina ukuta wa gati wenye urefu wa mita 385 unaoweza kutia nanga meli mbili na chombo kimoja cha mwambao kwa wakati mmoja. Kina cha meli ni mita 9.85 nakutokana na vifaa vya sasa vya kuongozea meli vinavyotumia umeme wa jua, meli zitaingia muda wote (saa 24)

Vifaa

Nyenzo za kushughulikia shehena ni pamoja na zana mbalimbali za kupakilia, kupakulia na kupanga shehena kama vile 1 Mobile Harbour Crane 100 tonnes, 2 Reach Stacker 45 tonnes each, 1 Front Loader 42 tonnes, 2 Mobile Cranes 50 and 25 tonnes, 3 Empty Handler, 8 forklifts 16 tonnes, 5 tonnes and 3 tons, 6 Terminal Tractors, 2 Hoppers and 4 Grabs. Marine crafts available at the Port are 1 Tug Boat and 1 Mooring Boat.

Bandari ya mtwara ina vifaa vingi na imejiandaa kushughulikia aina zote za pia tunafanya kazi saa 24 siku saba kwa wiki.

Uhifadhi

Kuna mabanda mawili ya shehena zinapitia Nchi nyingine yenye uwezo wa kuhifadhi takribani tani 12,500

Uwezo wa Sasa

Bandari ya Mtwara inaweza kushughulikia tani 400,000 za shehena zinazosafirishwa nje na zinazoagizwa kwa mwaka. Bandari hii hasa kwa bidhaa za kawaida.

 

Contact

Meneja wa Bandari Mtwara,
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
S.L.P 530,
MTWARA, Tanzania

Simu. +255 (23) 2333125
Faksi +255 (23) 2333153
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.