Bandari Ziwa Nyasa

Bandari kuu ziwa Nyasa Mbamba bay na Itungi /kiwira. Bandari ya kiwira imeanzishwa kuwa kituo cha shehena. Ina gati na ngazi ya muda ya kushukia na kupandia Bandari ya Kiwira ina mitambo ya kushughulikia shehena kama vile Winchi itembeayo , Foklifti na Vinyakulio kwa sasa bandari hii inapokea meli mbalimbali kutoka Malawi zinazo pakia magharibi ya cliniliki ya kusafirishwa nje. Bandari ya Kiwira ni maskani ya meli ndogo za mizigo za MV. RUVUMA NA MV NJOMBE zinazo milikiwa na TPA.

Program za Maendeleo

 • Meli moja ya abiria na mizigo ianayotarajiwa kuzinduliwa mwisho wa mwaka huu.
 • Ununuzi vifaa viwili vya kupakulia na mizani mbili za kupimia magari uko mbioni.

VIfaa vya bandalrini

Matokeo ya mizigo hadi 2028

 • Inakadiriwa tani 10,000 kwa Bandari ya itungi
 • Inakadiriwa tani 150,000 kwa bandari ya kiwira
 • Inakadiriwa tani 100,000 kwa Bandari ya Ndumbi
 • Inakadiriwa tani 50,000 kwa Bandari ya Mbamba Bay

Vifaa

 • Meli ndogo mbili zenye thamani ya bilioni 10.2
 • Winchi moja itembeayo
 • Kizoa taka chini ya maji kwa kusimamia kuna Fokolifti mbili

Miradi Iliyotekelezwa

 • Ukarabati wa Bandari ya Itungi
 • Utengenezaji wa nyenzo za kushughulikia abiria / shehena katika Bandari ya Kiwira
 • Ukarabati wa bandari Mbamba bay
 • Uendelezaji wa bandari ya Ndumbi
 • Ujengaji wa maeneo ya kupandia na kushukia abiria bandari mbalimbali wanakofikia.

Bandari Nyengine zilizoko ziwa nyasa

BANDARI YA MBAMBA BAY

Details

Bandari ya Mbamba bay ina Gati linalofaa kwa mizigo midogo . Bandari itapangiwa kuhudumia mahitaji yanayo ongezeka hasa baada ya kujengwa kwa meli mpya pia uendelezaji wa ukanda wa mtwara (Mtwara Corrdon) utaratibu wa upataji ardhi unaendelea kwa lengo la kupata eka 128 zitakazo wezesha ujenzi nyingine za Bandari.

Ukarabati wa Mbamba Bay

 • Utenegenzaji wa Gati la shehena kavu.
 • Uendelezaji wa Magati wawili/ Shehena zilizotenganishwa.
 • Ununuzi wa Winchi moja itembeayo

BANDARI YA NDUMBI

Details

Bandari ya Ndumbi inafanya miradi mingi ikiwemo ujenzi wa Gati wa sehemu ya kushukia. Ununuzi wa kipakizi chenye magurudumu kuchora kasha upakiaji wa shehena ya mkaa ya mawe unaendelea .Bandari ya Ndumbi imeonekana kuwa bandari mhimu sana iliyojengwa kimkakati kwa usafirishaji wa makaa yam awe. Kwenada Bandari ya Kiwira na Bandari ya Malawi kama vil Monkey bay na Chipoka.

Ukarabati wa Ndumbi

 • Uengenezaji wa magati mawili ( jumla mita 20)
 • Ununuzi wa Winchi mbili zitembeazo

BANDARI YA ITUNGI

Details

Bandari ya Itungi imelengwa kuwa kituo cha abiria kitakacho shughulikia shehena ndogo ndogo. Bandari hii inagati lenye urefu wa mita 70, ni ofisi kuu ya Bandari za ziwa Nyasa. Inakadiliwa na tatizo la mchanga wa tope unaothiri njia ya kuingilia Bandarini hata hivyo utaratibu wa kudhibiti unaonesha mafanikio . Bandari ina mtambo wa kusafisha taka chini ya maji naa hivyo kuwezesha kina cha maji kuongezeka katika mkondo wa kuingilia upande wa Gati.

Ukarabati wa Itungi

 • Utengenezaji wa magati mawili (jumla mita 120)
 • Ununuzi wa winchi mbili zitembeazo
 

Mawasiliano

Meneja wa Bandari Ziwa Nyasa,
Mamlaka ya Bandari (TPA),
S.L.P 400,
Kyela, Tanzania

Simu: +255 (0) 732 951744
Faksi: +255 (0) 754 311862
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.