Usalama na Ulinzi

Ili kuhamasisha usalama na Afya ndani ya eneo la Bandari, kunahitajika nidhamu ya hali ya juu kwa watumiaji wote wa Bandari. Ifuatayo ni miongozo itakayofuatwa kwa madhumuni ya kutii sheria za usalama.

Safety Ribbon TPA sw

Alama za Usalama

Kila mfanyakazi ni lazima afuate alama za usalama zilizowekwa kwenye maeneo mbalimbali Bandarini. Kwa mfano alama ya utelezi, kipito cha reli n.k. Kutofuata alama hizi kutasababisha ajali na ukigundulika umekiuka sheria za usalama za TPA, hatua kali za nidhamu zitachukuliwa.

Marufuku Kuendesha Kasi

Fuata Sera ya Usalama na Afya ya TPA, ili kuboresha usalama na Afya yako, usizidishe mwendo wa zaidi ya 20km kwa saa unapoendesha chombo cha moto ndani ya eneo la bandari. Katika eneo la Bandari kuna mitambo mikubwa ambayo daima ipo kazini, kwahiyo mwendo kasi unaweza kusababisha ajali.

Kuegesha

Hutakiwi kuegesha chombo cha moto kwenye njia ya reli kwani huweza kuhatarisha maisha na mali za wateja. Hivyo basi usizibe barabara yoyote ndani ya eneo la Bandari ili kuruhusu magari mengine na ya zimamoto kuweza kupita kwa urahisi na haraka wakati wa dharula.

Mavazi ya Usalama

Wafanyakazi wote watakaokuwa wanashughulikia shehena ni lazima waelewe kwa ukamilifu au kupata mafunzo ya jinsi ya kujilinda na kujikinga dhidi ya ajali na matukio mbalimbali hatarishi. Tumia mavazi halisi ya usalama nyakati zote unapokuwa kazini kwenye shughuli za Bandari. Mavazi haya ya usalama ni kama vile fulana zinazo akisi mwanga, mabuti, viatu vya usalama, kofia ngumu na mengineyo. Kwa hiyo kila mfanyakazi ni lazima avae Vifaa vya Kinga vya Kibinafsi (PPE) wakati wote wanapokuwa eneo la Bandari. Kushindwa kufanya hivyo itakuwa kinyume na sheria za usalama za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kusababisha adhabu kwa kutofuata sheria hizo.

Kizima Moto

Tumia vifaa sahihi vya kuzimia moto na hakikisha moto umezimika. Vifaa vya kuzimia moto vipo kila mahali pa kujazia mafuta kwa urahisi na uharaka wa kukabili moto mahali hapo. Aina ya vifaa vya kuzimia moto ni lazima viwe Kemikali Kavu ya Unga (Dry Chemical Powder) au Kaboni Dioksaidi (Carbon Dioxide) au Povu (Foam). 

Idara ya tahadhari ya majanga ya moto, Afya na mazingira itawapanga wazima moto kuwa tayari wakati wote wa utendaji kazi.

Mawasiliano

Iwapo utaona moto mahali popote eneo la bandari jaribu kuuzima kwa kutumia vifaa vya kuzimia moto vilivyopo na iwapo moto utaongezeka, usiendelee kuuzima kwa kutumia kifaa cha kuzimia moto ulichonacho bali piga simu kituoni kwa Na. 2116287 au 0755195896 au wasiliana na msimamizi wako wa kazi au mlinzi aliye karibu nawe. Kwa kutumia Radio Call yako toa taarifa ya ajali au tukio lolote hatarishi haraka kwenye chumba cha kudhibiti moto au piga kelele za moto ili kuwezesha wengine kuelewa na kuondoka haraka katika eneo la tukio.

Kujaza Mafuta na Kuwasha Gari

Kusudio la kutaka kujaza gari mafuta ni lazima litolewe taarifa kwa Meneja wa Bandari na idara ya Tahadhari ya Majanga ya Moto, Afya na Mazingira. Unapofanya miadi ya siku ya kujaza mafuta kiasi cha mafuta kinachotajwa kutumika ni lazima kioneshwe kwenye barua ya maombi kwa idara ya Moto Bandarini, Afya na Mazingira. Zingatia kuwa shughuli za kujaza mafuta ni lazima zifanywe mahali  pa wazi au neo la kukwepa moto na vifaa vya kujaza mafuta vinavyofaa kama (nozeli za kujazia mafuta) vitumike, hakikisha kuwa hakuna umwagikaji wa mafuta wakati wa kujaza mafuta kwenye gari.

Iwapo eneo limemwagika mafuta ni lazima lisafishe na iwapo hukulisafisha sheria za usalama za TPA zitatumika kukuadhibu, hakikisha kuwa vyombo vya kuchotea mafuta kutoka kwenye gari la mafuta kwenda kwenye magari ni sahihi kwa aina ya mafuta kama Petrol au Dizeli. Kujaza mafuta kwa kutumia vyombo vilevile kwa Petrol na Disel au kinyume chake havitaruhusiwa kwa sababu itasababisha hitilafu kwa injini. Kujaza mafuta kwa utaratibu huo ni kinyume na kanuni za usalama za TPA zitakazo sababisha adhabu na faida kwa uharibifu wa Gari.

Wakati wa kujaza mafuta injini ya gari ni lazima izimwe, simu za mkononi zizimwe na kuvuta sigara ni marufuku, tenganisha magari yote yanayobeba vyombo vya mafuta na magari mengine. Tenganisha vyombo vya kubebea mafuta na cheche za moto (kama Betri), unapoendesha gari na kubaini kuwa gari lako limeshika moto tafadhali usiingie kwenye maegesho yeyote ya Gari au kujichanganya na wengine kuepuka kueneza moto kwa magari mengine.