Huduma Shirikishi

01

Polisi na Zimamoto

Timu zetu za polisi na zimamoto zinapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki ili kujibu dharura yoyote bandarini na maeneo ya jirani. Kikosi chetu cha zima moto kinachofanya kazi kikamilifu na chenye vifaa vya kutosha kinajumuisha wataalamu wa uokoaji wenye uzoefu, wakiwa na vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu  ili kukabiliana na chochote kinachotokana na moto au milipuko inayotokana na hatari za kemikali na kibayolojia.Kikosi hiki hufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuhakikisha wafanyikazi, wageni na watumiaji wengine wa bandari wamejiandaa vyema kwa tatizo lolote la dharura. Mazoezi hayo hutumika kupima muda wa kukabiliana na hali hiyo na kutumika zaidi kuwafunza wahudumu wa dharura, wafanyakazi na watumiaji wa bandari ili kudumisha hali ya utayari na ufahamu mara kwa mara. Kikosi hiki pia kinashiriki katika juhudi za kuzima moto nje ya maeneo ya bandari kwa kushirikiana na mamlaka za mitaa husika.

02

Timu za Matibabu na Gari za Kubeba Wagonjwa

Timu ya matibabu ya TPA imejipanga kukabiliana na dharura ndani na maeneo ya karibu na bandari. Timu zinafanya kazi na afisa mkuu wa matibabu ili kuhakikisha kuwa wafanyikazi na watumiaji wengine wowote wa bandari wako katika hali nzuri ya kiakili na kimwili.Timu ya matibabu ina kituo maalum cha afya chenye vifaa vya kisasa na wataalam  wenye uwezo wa kufanya upasuaji wa kuokoa maisha.Pia kuna huduma ya ambulensi ya saa 24 ambao wako tayari kuhudumia wagonjwa wakati wowote. Pia kuna kituo cha mazoezi ya viungo chenye vifaa kamili vya mazoezi ya mwili na wakufunzi wa kitaalamu ili kuwaweka sawa wafanyakazi na wasiwe na msongo wa mawazo na magonjwa nyemelezi.

03

Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, Maji katika Gati