Usalama wa meli yako wakati inapoingia kwenye Bandari yetu yoyote ni kipaumbele chetu cha kwanza. Tunatoa huduma mbalimbali kwa vyombo vyote vinavyoingia kwenye Bandari. TPA inahakikisha usalama wa chombo chako wakati wote meli inapotia nanga na inapoingia gatini.

Huduma
Boti

Uongozaji Meli

Huduma ya mfumo wa safari za vyombo vya majini (VTS), uongozaji wa vyombo vya majini vinapoingia na kutoka bandarini zinapatikana kwa saa 24 kwa meli za makasha, magari (RORO) na za bidhaa za kawaida, za mafuta – KOJ zinapoingia na kutia nanga mchana tu na kutweka wakati wowote.

Uvutaji Meli

Kuna vyombo vinne (4) vya uvutaji na uegeshaji meli gatini, vikiwemo A50 na 55 za kuvuta kwa kizuizi

  • Vikisaidia meli kuingia na kutoka kwa kutumia vyombo viwili vya kuvuta.
  • Vyombo vya kuvuta na kusukuma

Kufunga / Kufungua Kamba ya Meli

Kufunga au kufungua kamba ya meli katika gati kwa kutumia boti ambazo zinapatikana katika gati. Kwa meli ambazo zinafunga gati la SPM zinatumia boti moja kwaajili ya kutoa huduma na boti ingine kwaajili ya kusukuma Meli.