

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuujulisha Umma, Wateja na Wadau wa Huduma za Kibandari wa ndani na nje ya Tanzania kuwa, kutakuwa na maboresho ya mfumo wake wa Uendeshaji Bandari (TOS) siku ya tarehe 11 April 2025 saa 4 usiku hadi saa 7 usiku. Maboresho haya yataathiri huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa huduma za meli, vilevile bandari ya Tanga na Mtwara kwa huduma za meli na mzigo.

Tanzania Ports Authority (TPA) would like to inform it's esteemed Customers, Stakeholders and the Public, in and outside the United Republic of Tanzania that, there will be an upgrade to its Terminal Operating System (TOS) on 11th of April 2025, from 10:00 pm to 1:00 AM. This upgrade will affect services at the Dar es Salaam port for vessel operations only and services at the Tanga and Mtwara ports for both vessel and cargo operations.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Bandari mpya wa Mbamba Bay iliyopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma unakamikika kwa wakati na kwa ubora.
Akizungumza tarehe 05 Aprili,2025 baada ya kutembelea na kukagua mradi huo mkubwa na wa kimkakati, Mhe. Balozi Nchimbi amesema kukamilika kwa Bandari ya Mbamba Bay, kutaimarisha zaidi Biashara katika ukanda wa mikoa ya kusini na nchi jirani za Malawi na Msumbuji.“
“ Mradi huu ni muhimu na faraja kubwa kwa wana Nyasa na unasubiriwa kukamilika kwake. TPA hakikisheni mnausimamia kwa nguvu zenu zote kwani ni Jambo Jema kwa maendeleo ya nchi yetu.” Amesema Mhe. Balozi Nchimbi.
Mhe.Balozi Nchimbi pia ameipongeza Menejimenti ya TPA kwa kuusimamia vyema Mradi huo muhimu na wa kimkakati ambao anasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatoa umuhimu wa pekee katika kukamilika kwake.
Mapema akitoa maelezo ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mbossa, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka Mdima, amesema mradi huo utakaojengwa kwa miezi 24, unatarajia kukamilika kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
Amesema ujenzi wa Bandari ukikamilika utafungua biashara kati ya Tanzania na nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji na kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar-es-Salaam, kuongeza ufanisi katika Bandari ya Mtwara na kuimarisha kiuchumi ushoroba wa kusini.
Mradi huu unajengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 49,700 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 81 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 26 na unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Jiwe la msingi la usanifu na Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay, liliwekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba 25, 2024.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ( Kulia) akimkabidhi Tuzo ya shukurani kwa kutambua mchango wa TPA kufanikisha Mkutano Mkuu Maalum wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri ( TEF) kwa Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA), Bw. Leonard Magomba( wa pili kushoto) ambaye alipokea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Bw. Plasduce Mbossa, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu Maalum wa mwaka wa TEF, tarehe 4 Aprili,2025 Mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu huo Maalumu ambapo amesisitiza umuhimu wa vyombo vya Habari katika kukuza maendeleo ya nchi. Pamoja na mambo mengine, wanahabari hao waliutumia Mkutano Mkuu huo Maalum kufanya uchaguzi wa uongozi wao mpya.
- TPA YASHIRIKI MAJADAILIANO YA KUKABIDHANA ARDHI ZAUENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI KAVU KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA KONGO
- ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) WA UKAGUZI WA DMGP
- TPA YASHIRIKI EAST AFRICA CARGO CONNECT SUMMIT JIJINI DAR ES SALAAM
- BANDARI YA MTWARA YAONGEZA KWA UFANISI WA KUHUDUMIA SHEHENA MCHANGANYIKO IKIWEMO ZA KEMIKALI