BODI YA WAKURUGENZI URC WATEMBELEA BANDARI YA DAR ES ALAAM

Bodi ya Wakurugenzi na Menejiment ya Shirika la Reli kutoka nchini Uganda wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ndg. Al -Hajji Abdallatiff D. Wangubo, leo tarehe 27 Mei, 2025 wametembelea bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala ya muunganisho wa njia mbalimbali za usafirishaji pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda
Bodi hiyo imepokelewa na Mkurugenzi Wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.