Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isaak Kamwelwe (MB), ameagiza wahitimu 196 wa Chuo cha Bandari (181 wa Stashada na 15 wa Astashahada), kupewa nafasi za ajira katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufuatia kufanya vizuri kati fani za shughuli za Bandari ili kuziba upungufu wa Wafanyakazi uliopo.

Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 25, 2018 wakati wa kuwatunikia Astashahada na Shahada jumla ya wanafunzi 196 katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha Bandari.

Wahitimu hao wamefuzu katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na Usimamizi wa shughuli za Meli na Bandari, Uhandisi na usimamizi wa matengenezo ya mashine, Zimamoto na Usalama, usimamizi wa Wakala wa Forodha na Usafirishaji wa mizigo pamoja na Usimamizi wa Mipango ya Uchukuzi na Usafirishaji.

KATIKA PICHA NI MATUKIO MBALIMBALI KUHUSIANA NA MAHAFALI HAYO.

PIC 1

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isaac Kamwelwe (MB) kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA, Prof. Ignas Rubaratuka.

PIC 2

Wanafunzi waliomaliza Astashahada na Stashahada wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali.

PIC 31

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akimkabidhi zawadi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isaac Kamwelwe (MB) huku akishuhudiwa na Wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha Bandari.

PIC 4

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isaac Kamwelwe (MB), Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko na Mkuu wa Chuo cha Bandari, Dkt. Joseph Kakeneno wakifuatilia matukio mbalimbali katika mahafali hayo.