Viongozi wa Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa nyakati tofauti wametembelea Banda la TPA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ( Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dkt. George Fasha na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed, wameeleza kuridhishwa kwao na elimu ya kuhusu shughuli za kibandari inayotolewa bandani hapo na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi.

Banda la TPA katika maonesho ya Sabasaba lipo Katika Kitalu namba 42 Mtaa wa Mataifa ambao pia wapo Waendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Kampuni za DP World na TEAGTL.

Bandari ya Mtwara imeendelea kuhudumia meli kutoka nchi mbalimbali ambapo tarehe 3 Julai 2025 imepokea meli ya MV SEA ARIES kutoka nchini China.

Meli hiyo imebeba tani 5,744.526 za shehena ya mizigo mchanganyiko ikiwemo magari, mitambo na vifaa kazi vya Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao.


Mamia ya Wananchi na Wadau wa Bandari wamejitokeza kwa wingi katika Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ( Sabasaba) ili kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali za utekelezaji bandarini na kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mamlaka.






Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara ameongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (UE) na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kikilenga kuangazia maeneo muafaka ya kushirikiana.

Akifungua Kikao hicho kilichofanyika Julai 3,2025 Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam, Prof. Kahyarara ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio ya Serikali katika sekta ya Uchukuzi hususani bandari, ujenzi wa viwanja vya ndege na reli ya mwendokasi (SGR).
Katika salamu zake za ukaribisho Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw.Plasduce Mbossa alielezea kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) na namna ulivyoongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa Nchi na Sekta ya Umma Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afika Bw.Christian Elias amesema Umoja wa Ulaya ni mshirika wa miaka mingi wa Tanzania katika Maendeleo akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukuza na kuimarisha uchumi.

- KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI ATEMBELEA BANDA LA TPA, DP WORLD NA TEAGTL KATIKA MAONESHO YA SABASABA
- TPA ICT SYSTEMS SCHEDULED DOWNTIME
- TPA YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MABAHARIA, DUNIANI ZANZIBAR
- HONGERA KWA MHA. MACHIBYA MASANJA KWA KUTEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC)
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"