Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu, ametembelea Banda la TPA na kupongeza ushirikiano uliopo kati ya TPA na wawekezaji.

Akiwa kwenye Banda la TPA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini,Dar es salaam , Balozi Mangu amesema TPA imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu ya Bandari ili kuongeza shehena na ufanisi kwa ujumla.

Kwa kushirikiana na wawekezaji kampuni ya DP World na Tanzania East African Gateway Terminal Limited(TEAGTL) ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam umeimarika kwa kiwango kikubwa na sasa bandari hiyo inaweza kuhudumia meli kubwa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanikiwa kuibuka mshindi wa pili katika tuzo ya Mwezeshaji wa Biashara na Uwekezaji wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, IJP (Mstaafu) Balozi Ernest Mangu amewapongeza Wafanyakazi wa Mamlaka na kuwataka kutumia ushindi huo kama chachu ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt.Baraka Mdima amewapongeza Wafanyakazi kwa ari kubwa waliyonayo katika kutumikia wateja na kuwataka kuzidisha ari ili kuleta tija zaidi

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amewataka Watanzania kutumia ushiriki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kama fursa ya kuuliza na kupata majibu sahihi ya maswali kuhusu shughuli zote za kibandari.

Mhe.Mwinjuma ametoa kauli hiyo Julai 6 2025, alipotembelea banda namba 42 la TPA lililopo Mtaa wa Mataifa katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kufanya maboresho katika miundombinu ya kuhudumia shehena katika Bandari zote nchini.

Nahodha. Mandia ametoa kauli hiyo Julai 05,2025 alipotembelea banda la TPA katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

- VINGOZI WA MENEJIMENTI YA TPA WATEMBELEA BANDA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
- MV SEA ARIES INAENDELEA KUHUDUMIWA BANDARI YA MTWARA IKIBEBA MITAMBO NA VIFAA VYA MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA KISIWA MGAO
- MAMIA WATEMBELE BANDA LA TPA KATIKA MAONEHSO YA SABASABA KUPATA ELIMU KUHUSU SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIBNDARI
- KARIBU BANDA LA TPA DAR ES SALAAM INTERNATIONAL TRADE FAIR (DITF), KARIBU TUKUHUDUMIE
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"