Katibu Mkuu wa Chama cha Usimamizi wa Bandari Mashariki na Kusini mwa Afrika (Port Management Association of Eastern and Southern Africa-PMAESA) Kanali Andre Didace Ciseau amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kikao kilicholenga kuimarisha uhusiano baina ya pande hizo mbili.
Kanali Ciseau amesema PMAESA inatambua na kuthamini mchango wa TPA kama miongoni mwa taasisi zenye uwezo mkubwa kiutendaji katika Ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika.
Akizungumza katika Kikao hicho Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka Mdima ameeleza mipango ya muda mfupi na mrefu ya TPA na utayari wa Mamlaka kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na PMAESA.




Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma kwa nyakati tofauti wametembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) katika Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayofikia tamati leo katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kuipongeza Mamlaka kwa ufanisi na mchango wake kwa Taifa kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu J. Suluo ametoa pongezi zake kwa kusema wanatambua na kuthamini mchango wa TPA katika uchumi na kijamii.
Naye Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware,amesema anatambua mchango wa TPA kwa uchumi wa nchi na umuhimu wa bidhaaa zinazoingia nchini kukatiwa Bima.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bwa.Salim Msangi ameipongeza TPA kwa ufanisi wa kuhudumia shehena.









Chuo cha Bandari kinaendelea kutumia fursa ya ushiriki katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kukutana na kutoa maelezo ya mafunzo yatolewayo na umuhimu wake,kwa wazazi na wanafunzi wa shule mbalimbali zilipo mjini Dodoma na mikoa ya jirani waliotembelea banda la TPA lililopo viwanja vya Nzuguni




Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo ametembelea Banda la Bandari ya Mtwara katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) ambayo yamehitimishwa rasmi tarehe 08 Agosti, 2025 katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mhe.Dkt. Jafo ameelezea kuvutiwa na utayari wa Bandari ya Mtwara katika kuhudumia shehena mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kama korosho.
Aidha, ameipongeza Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kufanya maandalizi mazuri ya maonesho hayo ambapo yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa Wananchi.


Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Dkt. Baraka Mdima ( Wa pili kulia aliyevaa miwani) anahudhuria Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zisizo na Bahari ( LLDC3) unaofanyika mjini Awaza, Turkmenistan kuanzia Agosti 5 hadi 8 ,2025.
Mkutano huo unalenga kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Vienna wa 2014- 2024 na kuweka ajenda mpya ya maendeleo jumuishi kwa miaka kumi ijayo, huku ukijadili changamoto mbalimbali zikiwemo gharama kubwa za usafirishaji, utegemezi wa nchi jirani na miundombinu kwa nchi zisizo na Bahari.

- MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA BANDA LA BANDARI YA TANGA MAONESHO YA NANE NANE MOROGORO
- MKUU WA MKOA MTWARA ATEMBELEA BANDA LA MTWARA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA MKOANI LINDI
- NAMPORT WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- WAIRI MKUU MSTAAFU AWASII WAFANYABIASHARA WA MAZAO KUTUMIA BANDARI YA TANGA NANE NANE
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"