MKUU WA MKOA MTWARA ATEMBELEA BANDA LA MTWARA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA MKOANI LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawalla, tarehe 6 Agosti 2025, ametembelea banda la Bandari ya Mtwara katika maonesho ya 12 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo vilivyopo Mkoani Lindi.
Mhe. Sawalla amevutiwa na utaratibu unaotumika kutoa elimu ya masuala ya Bandari kwa wadau mbalimbali wanaotembelea banda hilo. Vilevile, amesisitiza kuendelea kujiweka tayari katika kuhudumia shehena ya korosho katika msimu wa mwaka 2025/26.