Select your language

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Namibia (NAMPORT) ambao upo Nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku mbili, ukiwa na lengo la kujifunza kuhusu  Shughuli za utekelezaji Bandarini na utendaji wa kimajukumu wa TPA. 

Ujumbe huo wa Maafisa 13 kutoka NAMPORT, umeongozwa na Afisa Rasilimali Watu Mkuu Bi. Johana Hatutale na umepokelewa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA Dkt. George Fasha kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mbossa.

Maafisa hao pia wamepata fursa ya kujifunza kuhusu usimamizi wa rasilimali watu, uboreshaji wa miundombinu ya Bandari na mbinu bora za utoaji huduma kwa wateja na pia utatembelea Chuo cha Bandari (Bandari College) kwa ajili ya kuona namna Tanzania inavyowekeza katika maendeleo ya rasilimali watu kwa ajili ya sekta ya bandari.

Ziara hii ni sehemu ya ushirikiano wa kimataifa wa TPA katika kubadilishana uzoefu, kukuza ufanisi na kuendeleza diplomasia ya bandari Barani Afrika.