TPA YAIBUKA MSHINDI WA PILI KATIKA TUZO YA MWEZESHAJI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WAKATI WA MAONESHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanikiwa kuibuka mshindi wa pili katika tuzo ya Mwezeshaji wa Biashara na Uwekezaji wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, IJP (Mstaafu) Balozi Ernest Mangu amewapongeza Wafanyakazi wa Mamlaka na kuwataka kutumia ushindi huo kama chachu ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.
Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt.Baraka Mdima amewapongeza Wafanyakazi kwa ari kubwa waliyonayo katika kutumikia wateja na kuwataka kuzidisha ari ili kuleta tija zaidi