Wakufunzi na Wanafunzi kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi “National Institute of Security Studies - (NISS)” cha nchini Nigeria wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, tarehe 18 Juni, 2025 ili kujifunza namna Bandari inavyofanya kazi.

Ugeni huo uliongozwa na Naibu Kamanda Mkuu wa (NISS) Opoke Ngele na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Selemani Mkomi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Bw. Enock Bwigane, alipotembelea banda la maonesho la TPA Juni 18,2025, katika siku ya tatu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa, yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanaenda na kauli mbiu isemayo “ Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchagiza Uwajibikaji”.

- KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YA TEMBELEA NA KAGUA SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- MKURUGENZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM AONGOZA KIKAO KATI YA DP WORLD NA CHAMA CHA MAWAKALA WA MELI
- BANDARI YA MTWARA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA MADINI NA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA LINDI
- MKURUGENZI MKUU WA TPA BW. PLASDUCE MKELI MBOSSA KATIKA KIPINDI CHA TUNATEKELEZA TBC 1
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"