Select your language

Wakufunzi na Wanafunzi kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi “National Institute of Security Studies - (NISS)” cha nchini Nigeria  wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, tarehe 18 Juni, 2025 ili kujifunza namna Bandari inavyofanya kazi.

Ugeni huo uliongozwa na Naibu Kamanda Mkuu wa (NISS) Opoke Ngele na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa.