Select your language

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu, ametembelea Banda la TPA na kupongeza ushirikiano uliopo kati ya TPA na wawekezaji.

Akiwa kwenye Banda la TPA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini,Dar es salaam , Balozi Mangu amesema TPA imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu ya Bandari ili kuongeza shehena na ufanisi kwa ujumla.

Kwa kushirikiana na wawekezaji kampuni ya DP World na Tanzania East African Gateway Terminal Limited(TEAGTL) ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam umeimarika kwa kiwango kikubwa na sasa bandari hiyo inaweza kuhudumia meli kubwa.