WIZARA YA UCHUKUZI NA MENEJIMENTI YA TPA YAPOKEA UJUMBE KUTOKA UMOJA WA ULAYA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara ameongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (UE) na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kikilenga kuangazia maeneo muafaka ya kushirikiana.
Akifungua Kikao hicho kilichofanyika Julai 3,2025 Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam, Prof. Kahyarara ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio ya Serikali katika sekta ya Uchukuzi hususani bandari, ujenzi wa viwanja vya ndege na reli ya mwendokasi (SGR).
Katika salamu zake za ukaribisho Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw.Plasduce Mbossa alielezea kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) na namna ulivyoongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa Nchi na Sekta ya Umma Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afika Bw.Christian Elias amesema Umoja wa Ulaya ni mshirika wa miaka mingi wa Tanzania katika Maendeleo akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukuza na kuimarisha uchumi.