TPA YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MABAHARIA, DUNIANI ZANZIBAR

Viongozi na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kwa wingi kutembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani, yanayofikia kilele chake Juni 25,2025, katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Kisiwani Unguja, Zanzibar.
Katika maonesho hayo, TPA imetoa Elimu ya ubaharia kwa Wananchi na Wadau mbalimbali ambao wameipongeza Mamlaka kwa ufanisi mkubwa katika kuhudumia shehena kupitia Bandari zake.
Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yana kauli mbiu isemayo “ Bahari yetu, Wajibu Wetu, Fursa Yetu”.