KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI ATEMBELEA BANDA LA TPA, DP WORLD NA TEAGTL KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara amezipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) kwa kufanyakazi kwa kushirikiana na kuongeza ufanisi katika kuhudumia shehena.
Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo Julai 3,2025 alipotembelea banda la TPA lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.