Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati wa kongamano la pili la wiki ya kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na kujifunza lililofanyika mjini Arusha. Katika kongamano hilo ambalo lilienda samba samba na maonyesho kutoka taasisi za umma zilizopewa fursa ya kuonyesha na kuelezea shughuli zao mbalimbali liliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu. Pichani ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akipewa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za Mamlaka na Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiiano wa TPA, Bw. Leonard Magomba.