Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akionyeshwa maendeleo ya ujezi wa mradi wa Lagosa na mwenyeji wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Juma Kijavara. Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Lagosa iliyopo katika Kijiji cha Mgambo Wilayani Uvinza, mkoani Kigoma. Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amesema ujenzi huo unaogharimu TZS.15 bilioni tayari umefikia asilimia tisini na sita na kusisitiza ifikapo mwezi Aprili mwaka 2024 mradi huo uwe umekamilika, Aidha Prof.Mbarawa amesema uwepo wa bandari hiyo utachagiza ufanisi wa shughuli za kiuchumi hasa Kilimo ,uvuvi na biashara kwa wakazi wa mwambao wa ziwa Tanganyika ambao kupitia bandari hiyo wataweza kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwenda nje ya nchi. Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Juma Kijavara amesema Mamlaka imejipanga kukamilisha ujenzi huo haraka ili bandari hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi. Naye Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Bi. Dina Masamani ameishukuru Serikali kwa kujenga Bandari hiyo akisisitiza kuwa itawezesha wakazi wa eneo hili kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kusafirisha bidhaa kwenda Nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ipo umbali wa takribani 88km kutoka ilipo Bandari ya Lagosa. Waziri akikagua mradi Waziri akikagua mradi na wenyeji wake Muonekano wa Gati la Bandari ya Lagosa Muonekano wa Gati la Bandari ya Lagosa