Jumla ya tani 20,000 za madini ya Shaba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DCR) zinatarajiwa kusafirishwa kupitia Bandari ya Tanga kila mwezi. Kampuni kubwa ya uchimbaji Madini ya Shaba ya Cleancore kutoka (DCR) inatarajia kuanza kusafirisha sehena ya madini hayo kupitia bandari hiyo miezi michache ijayo. Hayo yalijulikana jana wakati wa ujumbe wa Kampuni hiyo uliongozwa na Mwenyeji wao ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bi. Anjelina Ngalula.ulipotembelea Bandari ya Tanga ili kujionea maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali. Mwisho