Bandari ya Tanga ipo katika hatua za mwisho kuandaa mchakato wa ujenzi wa magati meingine mawili mapya kwa ajili ya makasha na abiria. Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua eneo litakaljengwa magati hayo mawili mapya, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Juma Kijavara amesema mradi huo upo katika hatua za awali. “Magati hayo mawaili ni pamoja na gati la kwa ajili ya kuhudumia shehena ya makasha na gati kwa ajili ya kuhudumia abiria,” Mhandisi Kijavara. Mhandisi Kijavara amesema kwa sasa mradi huo upo katika hatua za awali za maandalizi ya kutangaza tenda katika mwaka wa fedha 2023/ 2024. Pamoja na kujipanga kwa mradi huu mkubwa, tayari Bandari hiyo imeshakamilisha maboresho ya miundombinu yake haswa ujenzi wa uboreshwaji wa magati, kuongeza kina na lango la kuingilia meli. Mradi huo, ulilenga kuongeza uwezo wa Bandari hiyo na kuboresha zaidi ufanisi wa utendaji wake katika kuhudumia wateja. Mwisho