Wizara ya Uchukuzi imeongoza kikao baina ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Africa Global Logistics Company (AGL) kutoka Rwanda kilichofanyika Novemba 24,2025 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi, Mhandisi Shomari Omari Shomari, amesema kikao hicho kimelenga kufungua fursa za ushirikiano katika sekta ya Uchukuzi na kibiashara kwa ujumla wake.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AGL Bw. Roger Nkubito amesema dhamira ya kampuni yake ni kuendeleza eneo la Bandari Kavu linalomilikiwa na Serikali ya Rwanda lililopo Isaka ili kuendelea kuimarisha Uchukuzi wa shehena kati ya Bandari za Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi.