Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani,  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Juni 03,2025 imeungana na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi kushiriki katika zoezi la kufanya usafi eneo la Uwanja wa Ndege wa Dodoma pamoja na maeneo yanayozunguka uwanja huo.

Maadhimisho haya ya kuelekea Siku ya Mazingira Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma chini ya kauli mbiu ya “Mazingira yetu na Tanzania ijayo Tuwajibike Sasa,dhibiti matumizi  ya Plastiki”yatafikia kilele Juni 05,2025. 

TPA ni mdau makini wa utunzaji wa mazingira ya bahari na maziwa katika maeneo yote zilipo Bandari zake.