Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mha. Dkt. Baraka Mdima, amepokea Cheti cha Pongezi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA kutoka Chuo cha Dar es Salaam Maritime Institute (DMI) katika Mahafali ya 21 ya Chuo hicho, tarehe 12 Disemba,2025 Jijini Dar es Salaam.

 Cheti hicho kimetolewa na DMI ikiwa ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa TPA katika kutoa nafasi za Mafunzo ya Vitendo (Industrial Practical Training – IPT) kwa wanafunzi wa chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Dkt. Mdima ameishukuru DMI kwa kutambua mchango wa TPA na kusisitiza kuwa Mamlaka itaendelea kushirikiana na Taasisi za elimu katika kukuza ujuzi na uwezo wa wataalamu wa sekta ya uchukuzi na usafirishaji.