Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Malima, amefunga rasmi mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) katika hafla ya utoaji vikombe kwa washindi iliyofanyika katika Uwanja Jamhuri mjini Morogoro Disemba 06,2025.

Katika mashindano hayo TPA imeibuka mabingwa katika michezo ya Netboli,Mpira wa Kikapu (Basketball) na kuvutana kwa Kamba kwa upande wa Wanaume,zote kwa mara ya tano mfululizo.

Kuvutana kwa kamba upande wa wanawake TPA ilishika nafasi ya pili,mbio za kupokezana vijiti wanawake na wanaume nafasi ya pili,huku kwa upande wa mpira wa wavu(wanawake), TPA ilinyakua nafasi ya mshindi wa tatu na Mpira wa kikapu(wanawake) nafasi ya pili.