Maofisa wa  Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na Megendo Zanzibar KMKM wakiongozwa na Mkuu wa Utawala na Fedha  Capt. Fadhil R. Mberua leo tarehe 21 Julai 2025 wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari ya Dar es Salaam kujifunza kuhusu  usalama wa Bandari , mawasiliano na namna ilivyojidhatiti katika kukabiliana na magendo katika kuhakikisha eneo la bahari  linakuwa salama. 



‎Ugeni huo ulipokelewa na Afisa Mwandamizi  wa Ulinzi na Usalama katika  Bandari ya Dar es Salaam Bw. Fortunatus Sandaria kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed.