Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Selemani Mkomi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Bw. Enock Bwigane, alipotembelea banda la maonesho la TPA Juni 18,2025, katika siku ya tatu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa, yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma. 

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanaenda na kauli mbiu isemayo “ Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na kuchagiza Uwajibikaji”.