Select your language

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya uchukuzi ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Dkt. Nchemba ametoa wito huo Oktoba 15,2026, wakati akifungua Mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri la Nchi Wanachama wa Shirika la Wanamaji la Afrika Mashariki, Kusini na Kaskazini ( MOESNA), uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuunganisha usafiri wa majini, barabara pamoja na reli kutapunguza muda na gharama za usafirishaji, huku kukirahisisha upatikanaji wa masoko kwa nchi za Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema maendeleo ya sekta ya uchukuzi ni msingi muhimu wa kukuza biashara, kuvutia uwekezaji, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi wa nchi za ukanda huo.