Select your language

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Dkt.Baraka Mdima amewataka Watumishi wapya wa Mamlaka hiyo kuzingatia dira,dhima, kanuni  na sheria katika kutekeleza majukumu yao.

 

Akizungumza wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo kwa Watumishi hao wapya yaliyofanyika Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam Machi 16,2026 ,Dkt.Mdima amesema mafunzo hayo yatawapa msingi muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

Katika salamu za ukaribisho Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw.Mbarikiwa Masinga amewaambia Watumishi hao kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha kujua vyema malengo na maono ya Mamlaka jambo litakalowawezesha kufanyakazi kwa weledi.