WAKUFUNZI NA MAFISA KUTOKA CHUO CHA MAFUNZO YA STRATEGIA WATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SAALAM
Wakufunzi na Maafisa Wanafunzi kutoka Chuo cha Mafunzo ya Strategia ya Ukamanda na Unadhimu cha Duluti (Arusha Command and Staff College) kilichopo Arumeru mkoani Arusha, wakiongozwa na Luteni Kanali Helmani Cosmas, tarehe 15 Juni 2026 wametembelea Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli za bandari pamoja na namna Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilivyojidhatiti katika kuimarisha ulinzi na usalama wa meli, mizigo na miundombinu ya bandari.Ugeni huo ulijumuisha Maafisa Waandamizi wa Kijeshi kutoka nchi za Misri, Rwanda, Ethiopia, Uganda, Malawi, Afrika Kusini, Nigeria, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, ambapo bandarini ulipokelewa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed G. Abed, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.Katika ziara hiyo, Maafisa hao walipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za uendeshaji wa bandari, mifumo ya usalama inayotumika kulinda meli na mizigo, pamoja na mikakati inayotekelezwa na TPA kuhakikisha bandari zinaendelea kuwa salama na zenye ufanisi katika kuhudumia biashara ya ndani na kimataifa.Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya bandari na kujionea shughuli za upakiaji na upakuaji wa shehena zinavyotekelezwa kwa kutumia teknolojia na mifumo ya kisasa inayoongeza ufanisi wa huduma bandarini.TPA ni mdau muhimu katika masuala ya ulinzi na usalama wa taifa kutokana na nafasi yake ya kimkakati katika kuwezesha biashara, uchumi na usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"