URC YAJIPANGA KUONGEZA SHEHENA KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Shirika la Reli Uganda (URC) limeeleza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano na sekta ya Uchukuzi nchini Tanzania kupitia usafirishaji wa shehena itokayo Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli ya Shirika la Reli nchini (TRC). Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya URC, Bw.Daudi Migereke katika kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Septemba 21,202.
Bw.Migereke amesema lengo la ziara ya Bodi ya Shirika hilo ni kuangalia namna ya kukuza na kuendeleza biashara ya Uchukuzi kwa faida ya Uganda na Tanzania. Mapema katika salamu zake za ukaribisho, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw.Abed Gallus Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, amewapongeza Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo kwa kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam. Aidha Bw.Gallus amesema Bandari ya Dar es Salaam imeshuhudia ongezeko kubwa la shehena katika miaka ya karibuni, hali ambayo imechagizwa na ushirikishwaji wa sekta binafsi na utanuzi wa miundombinu ya bandari uliofanywa na Serikali kupitia TPA.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"