Select your language

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuandaa mkutano muhimu uliowakutanisha Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali wanaotumia Bandari za Ziwa Viktoria, ili kujadili changamoto wanazokabiliana nazo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Amir Mkalipa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe.CP. Salum Hamduni, wakati akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara na Wadau wa Usafirishaji katika ushoroba wa Kati kilichofanyika Oktoba 13,2026 jijini Mwanza.

Mhe.Mkalipa amesema Mkutano huo usiishie katika kutambua  changamoto pekee bali uweke maazimio yanayotekelezeka na yakionyesha majukumu ya kila mdau na muda wa utekelezaji wa maazimio ya mkutano huo.

Awali katika hotuba ya ukaribisho iliyosomwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dkt.George Fasha kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA,alisema Mkutano huu umelenga kujadili changamoto zisizo za kiforodha na kuzipatia majibu.

Aidha Dkt.Fasha aliwataka washiriki wa Mkutano huo kujadili kwa namna itakayoleta ufumbuzi wa changamoto katika sekta ya uchukuzi.

Akizungumzia utendaji wa Bandari za Ziwa Victoria, Meneja wa Bandari hizo Bi.Rosemary Ndesamburo alisema ni kiungo muhimu cha biashara katika ushoroba wa kati na mwaka wa fedha uliopita 2025/2026 ilihudumia jumla ya tani 281,700,848 tofauti na mwaka uliotangulia ambapo walihudumia tani 210,205.29 ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.