Select your language

Wataalamu na viongozi kutoka Taasisi za Bandari ikiwemo ( NAMPORT) , Mapato (NAMPOL), Uhamiaji, Kitengo cha polisi wa INTERPOL na udhibiti wa matukio ya uhalifu baharini (NAMRA) kutoka nchini Namibia, tarehe 12 Oktoba 2026 wametembelea Bandari ya Dar es Salam katika ziara yao ya siku tatu kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maeneo ya kiutendaji na udhibiti wa uhalifu katika maeneo ya bahari na bandari.

Wageni hao wamepokelewa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw.Plasduce M.Mbossa.

Wataalamu hao pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kupata maelezo ya namna TPA inavyofanya kazi kwa ushirikiano na Taasisi mbalimbali za udhibiti na kupambana na uhalifu kwa ufanisi.

Aidha wameelezwa namna mradi wa mafunzo na kuwajengea uwezo wa kiutendaji wa IMO (2020-2024) ulivyowaongezea uwezo na umahiri watendaji wa TPA na vyombo vya ulinzi na udhibiti katika kutekeleza majukumu yao.

Wageni hao pia wametembelea na kuona utendaji wa ukaguzi wa kiulinzi na mifumo ya ulinzi saidizi katika mageti ya namba 2 na 3 na kupata maelezo kutoka kwa wataalamu namna shughuli zinavyoendeshwa katika maeneo hayo ya kiutendaji.