TPA YAPONGEZWA KWA MABORESHO YA BANDARI NDOGO YA MAFIA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imepongezwa kwa jitihada zake katika kuziboresha bandari ndogo ikiwemo ya Mafia ili kutoa huduma bora na kuziongezea uwezo kuhudumia meli kubwa zaidi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akimuwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Bashiru Ally Kakurwa (Mb) alipotembelea banda la TPA katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya Uhifadhi wa Bahari yaliyofanyika Wilaya ya Mafia kuanzia Tarehe 24 hadi 26 Septemba, 2026.
Mhe. Chande amepongeza kazi nzuri inayofanywa na TPA na kuitaka Mamlaka kuendelea kuiboresha Bandari ndogo ya Mafia iweze kupokea Meli kubwa zaidi kutokana na ukweli kwamba kwa Sasa Mafia inakua kwa kasi zaidi na mahitaji yanaongezeka.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Chande amepata nafasi ya kutembelea mabanda ya washiriki wa maonesho haya ikiwemo la TPA na kupata maelezo kuhusu Bandari ndogo ya Mafia kutoka kwa Msimamizi wa Bandari ya Mafia Ndg. Ramadhani Mkango juu ya Shughuli zinazoendeshwa na Bandari mdogo ya Mafia ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa Shehena za Mizigo, na Abiria.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"