Select your language

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mha. Ali Said Bakari, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kutekeleza sera ya bahari katika kuimarisha ulinzi na usalama katika bandari zake. Mhandisi Bakari ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda ya TPA wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Usafirishaji Majini Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Kijiji cha 
21, Tanga Mjini, ambapo alikuwa mgeni rasmi.  Amesema mafanikio katika sekta ya bandari yana mchango mkubwa katika kuboresha miundombinu ya bahari nchini pamoja na kuimarisha ulinzi kwa watumiaji wa bahari pamoja 
na shehena za wateja. Awali akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi,  Afisa Mkuu Masoko kutoka TPA Bw. Ally Tembele, ameeleza kuwa TPA inaendelea kuthibitisha kwa vitendo  utekelezaji wa Dira ya 
Maendeleo ya Taifa ya 2050 kwa kununua Boti mbili za kisasa za doria kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama majini                                                                                                                                                                                                
Boti hizo ambazo ni MV Lindo I na MV Lindo II zimeongeza ulinzi kwa watumiaji wa huduma za bandari, Meli na Shehena za wateja. TPA imeungana na taasisi zingine zinazohusika na sekta ya bahari nchini, katika kuadhimisha 
siku ya Usafirishaji Majini Duniani yenye kaulimbiu: “Kutoka Sera hadi Utekelezaji: Kuimarisha Ubora Katika Sekta ya Usafirishaji Majini.”