Select your language

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam wamefanya ziara ya siku moja katika mradi mkakati wa ujenzi wa matanki 15  kupokea na kusamba na mafuta uliopo kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed, Meneja wa Shughuli za Meli Bandari ya Dar es Salaam  Kapt. Peter C. John, amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuwawezesha Wajumbe wa Baraza hilo kupata uelewa juu ya mradi na maendeleo yake pamoja na kushauri mambo mbalimbali katika utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wa Msimamizi wa mradi huo Mha. Hamis H. Mbutu, ameshukuru ujio wa wajumbe hao ambao pamoja na mambo mengine  wamehainisha mambo mbalimbali na maoni yatakayoenda kuboresha utekelezaji  wa mradi huo.

Naye Meneja Utawala Bandari ya Dar es Salaam Bw. Juma Ng’oko akiongea  kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam, amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utawezesha upatikanaji wa mafuta kwa wakati, kupunguza gharama za uendeshaji na hatimaye kupungua kwa bei ya mafuta nchini.