TPA YAHAMASISHA UMOJA NA USHIRIKIANO KUPITIA MICHEZO YA INTERPORTS
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Queen Sendiga, ameipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kuwekeza kwenye ustawi wa Wafanyakazi wake kupitia Michezo ya Bandari.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Mussa Kilakala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, katika hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 19 ya Bandari (Interports Games) iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri.
Aidha Mhe. Kilakala amesema michezo inaimarisha afya za Wafanyakazi, kuleta Umoja na kuongeza utimamu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya ujenzi wa Taifa.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Meneja Utawala wa Bandari ya Dar es Salaam Bw.Juma Ng’oko, aliwaasa washiriki wote wa michezo hiyo kuzingatia nidhamu muda wote wanaposhiriki katika mashindano hayo.
Baada ya ufunguzi huo.mgeni rasmi alipata fursa ya kutizama mechi ya kandanda baina ya Bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar ambazo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu huku katika mchezo mwingine timu ya kabumbu ya Makao Makuu ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Bandari za Maziwa, ambao bao la Makao Makuu limefungwa na Mrisho Harambe.
Katika mchezo wa kuvutana kwa kamba ilishuhudia timu ya Wanawake ya Makao Makuu ikiwanyanyasa timu ya Bandari Mtwara kwa mivuto (2- 0) huku timu ya wanaume ya Makao Makuu ikitolewa jasho na Bandari Mtwara kwa mivuto yote miwili.
Timu za Kamba za Bandari ya Tanga wanawake na wanaume zimeshinda mechi zao dhidi ya Bandari ya Zanzibar.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"