Select your language

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Galus Abed,  tarehe 14 Oktoba, 2026 amewaongoza wafanyakazi wa bandari hiyo na wadau wake kufanya usafi katika Bandari na maeneo jirani katika Kampeni yenye kauli mbiu ‘ Ng’arisha Bandari, Usitupe Taka hovyo.

Bw. Abed amesema zoezi hilo ni sehemu ya mkakati wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania

 ( TPA) kutoa huduma katika mazingira safi na ni zoezi endelevu.

Hivyo, amesema kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi Wafanyakazi wa Bandari na Wadau wataungana kufanya usafi maeneo ya bandari na jirani.

 Amewaasa wafanyakazi na wadau kuzingatia usafi na kutunza mazingira, huku akisisitiza kwamba ajenda ya usafi itakuwa  ya kudumu katika vikao vya ndani na vya wadau.