Select your language

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kuimarisha uhusiano na wadau wake kwa kuwatembelea na kuwapatia tuzo ikiwa ni ishara ya kuthamini na kutambua mchango wao katika kukuza maendeleo ya bandari.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam Bw. Abed. G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduse M. Mbosa ametembelea na kukabidhi tuzo kwa Chama cha Waendesha Bandari Kavu Tanzania (CIDAT) pamoja na Chama kinachosimamia na kuwasemea Mawakala wa Forodha (TACAS).

Akikabidhi tuzo hizo, Bw. Abed amewashukuru wadau hao kwa ushirikiano wao ambao umechangia ukuaji wa bandari na ongezeko la shehena kufikia tani Mil. 33.7.

“Mmekua mkitoa mchango chanya katika kupokea na kuondoa shehena na kama mjuavyo bandari utendaji wa Bandari unategemea sana uwepo wa nafasi kwa ajili ya kuhudumia shehena, kwahiyo uwepo na ongezeko la bandari Kavu mmesaidia mizigo inayoongezeka kupata nafasi na kuvutia wateja zaidi na sasa TPA tunaongoza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki” amesisitiza Bw. Galus