TPA MTWARA YAIMARISHA MAHUSIANO NA WADAU WA MTWARA NA LINDI
Bandari ya Mtwara imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 kwa kuwashirikisha wadau wake katika Bandari za Mtwara na Lindi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano, kusikiliza maoni na changamoto zao pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa na Bandari.
Wakuu wa Wilaya za Mtwara na Lindi Bw. Bw. Abdallah Mwaipaya na Bi. Victoria Mwanziva, kwa nyakati tofauti, wameshiriki wameshiriki katika maadhimisho hayo wakitoa msisitizo kwa wadau kuendelea kushirikiana na Bandari kwa ukaribu zaidi na kuwasilisha changamoto zao kwa wakati ili ziweze kufanyiwa kazi.
Pia wamesisitiza umuhimu wa mawasiliano bora na mahusiano mazuri kati ya Bandari na wadau, huku akiwataka wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara kuhakikisha huduma bora kwa wateja haiishii kwenye Wiki ya Huduma kwa Wateja pekee, bali iwe sehemu ya utamaduni wa kila siku wa utendaji kazi.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Mtunze Sudi, alitoa shukrani kwa wadau kwa ushirikiano wao na kuahidi kuwa changamoto na maelekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili kuendelea kuboresha huduma za Bandari.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"