TPA KIVUTIO MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kuwa kivutio kikubwa katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo wananchi, wadau mbalimbali na washiriki wamaonesho hayo wamekuwa wakitembelea banda la mamlaka hiyo kupata taarifa na elimu kuhusu huduma na shughuli zinazotekelezwa na TPA.TPA inashiriki maonesho hayo yaliyoanza tarehe 16 Juni 2026 kwa lengo la kutangaza huduma zake, kuonesha mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa taifa pamoja na kuwasilisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya bandari kwa mwaka wa fedha 2025/2026.Kupitia banda lake, TPA imekuwa ikitoa elimu kuhusu huduma za bandari, maboresho ya miundombinu, matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena katika bandari mbalimbali nchini.Maonesho hayo yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”, ikiwa ni mwito kwa taasisi za umma kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia uwajibikaji, ushirikishwaji na uendelevu.Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Juni 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 23 Juni 2026.Ushiriki wa TPA katika maonesho hayo unaendelea kutoa fursa kwa wananchi na wadau kupata uelewa mpana kuhusu nafasi ya bandari katika kuchochea biashara, uwekezaji na maendeleo ya uchumi wa Taifa.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"