TPA IMEJIPANGA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ILI KUKIDHI MAHITAJI YA WATEJA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA ) IGP Mstaafu Balozi Ernest Mangu, ameseme wiki ya huduma kwa mteja inatoa fursa ya kufanya tafakari ya namna bora ya kutoa huduma kwa ufanisi.
Balozi Mangu ametoa kauli hiyo Septemba 5,2026 katika hafla ya ufunguzi wa wiki ya huduma kwa Wateja iliyofanyika katika jengo la Makao Makuu ya TPA (Bandari Tower, One Stop Centre ).
Aidha Balozi Mangu amesema bandari bila wateja ni kazi bure na kwahivyo TPA imejipanga kutekeleza majukumu yake zaidi ya kawaida ili kukidhi mahitaji ya wateja na wakati huo huo kuteleza malengo ya Dira 2050.
Katika salamu zake za kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Mkurugenzi Mkuu Bw.Plasduce Mbossa, amesema TPA ina dhima ya kuwa lango kuu la bahari linalotoa huduma fungamanishi za uchukuzi zenye hadhi ya Kimataifa.
Aidha Bw.Mbossa amesema katika kutimizi dhima hiyo TPA haitoishia tu kwenye kuhudumia meli na shehena kwa ufanisi bali itakwenda hatua za ziada kwa kutambua mahitaji ya wateja mapema,kuwapatia taarifa kwa wakati na kutatua changamoto kabla hazijaathiri biashara zao.
Awali katika salamu za utambulisho,Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw.Abed Gallus Abed alisema ushirikishwaji wa sekta binafsi katika Bandari ya Dar es Salaam umeongeza tija kubwa katika uhudumiaji wa shehena za wateja.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"